Saturday 6 February 2016

TACOMO; Waliojifungua watoto wenye vichwa vikubwa njooni

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Tanzania Community Media Organization (TACOMO), limewataka wazazi wote wenye watoto waliozaliwa wakiwa na vichwa vikubwa wasiozidi miaka miwili Tanzania bara, wajitokeze na watagharamiwa gharama za matibabu.

Shirika hilo ambalo lina makao makuu mkoani Mbeya na linafanya kazi Tanzania bara, limesema kuwa kansa ya watoto inatibika hivyo wazazi wasiwafiche watoto wao na kwamba shirika hilo kwa sasa linaendesha mradi wa kuwasaidia watoto wenye matatizo hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mbeya leo, Mkurugenzi wa shirika hilo ndugu Gordon Kalulunga, amesema shirika lao kwa kila mzazi atakayejitokeza atagharamiwa nauli ya kutoka popote Tanzania Bara na kuelekea katika Hospitali ya Taifa Muhimbili au Bugando Jijini Mwanza, ambapo akifika huko ataunganishwa moja kwa moja na marafiki wa shirika hilo ambao watampokea na mtoto kufanyiwa vipimo vya awali kisha upasuaji.

"Tafadhali, naomba vyombo vya habari tusambazieni taarifa hizi kwa watanzania wote. Kwanza kabisa tunaomba kila mwananchi atambue kuwa kuna shida duniani na tunapaswa kujaliana hivyo tunaomba michango ya hali na mali ya kuwawezesha watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na kuwasafirisha pia maana matibabu yanatolewa bure katika hospitali ya Bugando Mwanza na Muhimbili Jijini Dar e Salaam" alisema Kalulunga.

Alisema mwenye taarifa ya mtoto aliyezaliwa akiwa na kichwa kikubwa anaweza kuwasiliana moja kwa moja na uongozi wa shirika hilo kwa namba 0765 615858 na kwa marafiki ambao wanaguswa na suala hili la kusaidia wahitaji wanaweza kuchangia michango yao kwa namba 0754 440 749/0655 440 749 au 0765 615858 na kwa Akaunti benki ya NMB 

JINA LA AKAUNTI:  TANZANIA COMMUNITY MEDIA ORG
NAMBARI YA AKAUNTI: 62510007257
JINA LA BENKI: MICROFINANCE BANK (NMB)
JINA LA TAWI: USONGWE BRANCH

No comments:

Post a Comment