Friday 19 February 2016

Lishe hii hapa inamfaa mjamzito

Vyakula Muhimu Wakati wa Ujauzito

Lishe bora wakati wa ujauzito ni muhimu sana, kwani lishe hii hutumika kwa mama na mtoto anaendelea kukua tumboni. Kwa kawaida mahitaji ya chakula na virutubisho mwilini mwa mwanamke huongezeka wakati wa ujauzito na kadri ujauzito unavyoendelea kukua, virutubisho hivyo hutumika kujenga mwili wa mama na mtoto. 

Hivyo maamuzi ya lishe au lishe mama anayopata huathiri pia maendeleo ya mtoto anayekua mwilini mwake. Tutaona vyakula muhimu vya kuzingatia lishe bora wakati wa ujauzito na baadhi ya vitu vya kukwepa.


Mlo kamili (balanced diet), ni muhimu kwa ajili ya maendeleo mazuri ya afya ya mjamzito na mtoto tumboni. Pamoja na mlo kamili mjamzito hupewa virutubisho ziada (supplements) kwa ajili ya kuongeza madini kama ya chuma na Foliki. Mlo kamili unajumuisha vyakula vya wanga, protini, mafuta, vitamini, madini na maji kama inavyochambuliwa hapa chini;
Nafaka na Vyakula vya Wanga.
Vyakula hivi huupa mwili nguvu za kufanya kazi ikiwemo ukuaji wa mtoto tumboni. Vyanzo vya wanga ni kama nafaka mbalimbali(mahindi,mtama,ulezi n.k), viazi, ndizi, mihogo. Ni vizuri mjamzito awe anapata nafaka kamili(whole grains) kama mahindi, ngano na mchele usiokobolewa; cereals n.k.
Nyama, Samaki na Vyakula vya Protini.
Hivi ni muhimu kwenye kuujenga mwili, hasa kipindi cha miwezi wa 4 mpaka wa 9 ambacho viungo mbalimbali vya mtoto vinajengwa. Ni muhimu mama apate vyakula vya protini vya kutosha ili kuhakikisha ukuaji wa mtoto unaenda vizuri. 

Nyama za kuku, ng’ombe, mbuzi, senene, panzi na wanyama wengine ; vyanzo vya protini za mimea kama maharage, soya, njugu, njegere, karanga,korosho n.k . Samaki, maziwa, mayai ni vyanzo vingine vya protini muhimu.
 
 
Vyakula vya protini.

maziwa
Vyakula vya Mafuta.
Hutumika kwenye kuupatia mwili nguvu pamoja na ujengaji wa seli za mwili. Mara nyingi vyakula kama nyama, karanga, ufuta, alizeti,senene, panzi, samaki na matunnda kama maparachichi huwa na mafuta. Ni vizuri kutumia mafuta yatokanayo na mimea ili kupunguza mafuta yenye lehemu(cholesterol) nyingi.
Mboga za Majani na Matunda.
Matunda na mboga za majani ni sehemu muhimu sana ya mlo wakati wa ujauzito, kwani huupatia mwili vitamini, madini na kambakamba kwa ajili ya kulainisha chakula. Vitamini husaidia kuimarisha kinga ya mwili sambamba na ufanyaji kazi wa mwili.  Madini kama ya chuma, kalsiamu, zinki, madini joto(Iodine) na magneziamu ni muhimu kwa ukuaji salama wa mtoto tumboni mwa mama.
 
mboga za majani
 
Vitamini B9 (Foliki asidi) na madini ya chuma hutolewa kama virutubisho ziada kliniki wakati wa ujauzito ili kutosheleza mahitaji ya mwili na kuzuia hatari ya upungufu wa damu kutokea.

matunda
Maji
Maji ni muhimu kwenye mmenyenyo na unyonywaji wa chakula, pia husaidia kuzuia choo kigumu, mwili kuvimba na maambukizi ya mfumo wa mkojo (UTI). Inashauriwa mjamzito anywe maji si chini ya lita 2.3 kwa siku, yanaweza kuwa katika chai, juisi, soda, au maji yenyewe. Ni vema zaidi kama akinywa maji kama maji zaidi na kupunguza vinywaji kama soda.
Mfano wa Mpangilio wa Mlo.
Ili kuhakikisha mlo kamili mjamzito anaweza kufuata mfano wa mpangilio wa mlo ufuatao;
mpangilio wa chakula
Mfano,
  • Mlo wa Asubuhi:    A – Chungwa/ Embe/ Ndizi mbivu/ Parachichi,  B – Mkate/ Maandazi/ Chapati/ Vitumbua,Uji      C – Karoti    D – Mayai,    E – Maziwa/ Mtindi/ Siagi/ Maziwa ya  Soya
  • Mlo wa Mchana:     – Parachichi/ Papai/ Ndizi/ Embe na chungwa,  B – Ugali/ Wali/ Ndizi/ Makande/ Tambi          C – Mchicha/ matembele/ Mnavu/ Kisamvu/ Spinach/ Kabeji,      – Maharage/ Samaki/ Kuku/ Njugu/ Nyama/ Dagaa        E – Maziwa/ Mtindi/ Siagi/ Maziwa ya  Soya.
  • Mlo wa Usiku:        A – Parachichi/ Papai/ Ndizi/ Embe na Chungwa,   B – Wali/ Ndizi/ Viazi/ Tambi/ Chapati          – Mchicha/ Matembele/ Mnavu/ Kisamvu/ Spinach/ Kabeji,      – Maharage/ Samaki/ Kuku/ Njugu/ Nyama/ Dagaa           – Maziwa/Mtindi/Siagi/Maziwa ya  Soya.
Vitu na Vyakula vya kuepuka/kupunguza
  • Matumizi ya Pombe wakati wa ujauzito huathiri mtoto. Haishauriwi kutumia pombe kabisa!
  • Uvutaji Sigara
  • Kupunguza unywaji wa kahawa au vinywaji vyenye caffeine nyingi.
  • Samaki aina ya papa, swordfish, tilefish na king mackerel kwani wana mekuryi kwa wingi amabayo ni mbaya kwa afya.

VIJANA NCHINI WASHAURIWA KUWA NA MOYO WA KUJITOLEA KABLA YA KUPATA AJIRA RASMI


Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa nchini (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akisoma hotuba ya ufunguzi wa warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV) kwa niaba ya Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez.

Vijana nchini hususani wanaomaliza masomo ya vyuo wametakiwa kujijengea tabia ya kufanya kazi zinazokuwepo pindi wamalizapo masomo yao na isiwe mpaka kazi inayoanza na maslahi makubwa.

Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (National Information Officer-UNIC), Bi. Usia Nkhoma- Ledama aliyemwakilisha Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez katika warsha iliyozikutanisha taasisi mbalimbali zinazofanya kazi kwa kujitolea za vijana.

Bi Ledama, alisema kumekuwepo na kundi kubwa la vijana ambao wamekuwa wakihitimu masomo yao lakini hawajishughulishi na kazi yoyote lakini kuna wanaweza kutumia fursa zilizopo hata kwa kuanza kwa kujitolea na kupitia kwenye kazi hiyo akajifungulia milango ya mafanikio.

Ameongeza kuwa, Vijana wengi wamekuwa wakihitaji kazi ambazo zina maslahi makubwa pindi tu wanapoanza kazi kwa kipindi kifupi wapate maisha mazuri bila kutambua kuwa wanahitaji kufanya kazi kwa bidii na maisha mazuri ndiyo yanafuata.

“Ukitaka maisha mazuri lazima ufanye kazi kwa bidii sio unataka uanze kazi upange nyumba ya vyumba vitatu na ipo sehemu nzuri, ununue gari Mark X na mengine mazuri lakini lazima ufanye kwanza kazi,
“Vijana mnatakiwa kutambua kuwa ajira ni ngumu kupatikana hata kwa kuanza kufanya kazi kwa kujitolea bila malipo unaweza kuwa na juhudi na mwisho wa siku unakuwa na maisha mazuri,” alieleza Bi Usia Nkhoma Ledama.

Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa nchini (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akizungumza jambo katika warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV).

Na kuongeza kuwa vijana wengi wasomi hawajui faida za kuanza kwa kujitolea kuwa kunampa uzoefu na zaidi katika kuhudumia jamii kwa shughuli mbalimbali ambazo zinakuwa na kusudi za kuelimisha jamii kuhusu mambo mengi kwao pia kupata elimu mpya.

Kwa upande wake, Mwakilishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na Walemavu, Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Vijana, Bi. Esther Liwa amezishauri taasisi za vijana kuwa na utaratibu wa kutoa elimu kwenye maeneo ya wazi ili kupata nafasi ya kukutana na vijana wengi zaidi.

Alisema kuna kundi kubwa la vijana walio mtaani hivyo kufanya kwao maonesho ya wazi watapata nafasi ya kutoa elimu kwa vijana walio mtaani ambapo nao hawajapata elimu kuhusu kujiunga na taasisi hzio kwa kujitolea.

Aidha, aliwataka vijana kutumia vitu vilivyo na asili ya Tanzania kama utambulisho wao kama jina la warsha hiyo lilivyokuwa Kitenge – Africa – Volunteerism (KAV).
Afisa Mipango wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kujitolea (UNV), Stella Karegyesa akizungumza na wanafunzi kutoka vyuo mbalimbali (hawapo pichani) kuhusiana na shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika lake wakati wa warsha hiyo.
Baadhi ya vijana walioshiriki katika warsha ya Kitenge - Africa - Volunteerism (KAV) iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kazi za kujitolea miongoni kwa vijana, wa kwanza katika mstari wa mbele ni Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Vijana, Bi. Esther Liwa.

Warsha hiyo iliwakutanisha zaidi ya wanafunzi 100 wa vyuo vikuu walishiriki katika tukio hilo, wakajifunza na kuoneshwa kufurahishwa na kuhamasika na vijana wenzao wanaofanyakazi za kujitolea ambapo iliandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la kujitolea (UNV) ikiwa na lengo la kuhamasisha masuala ya kujitolea miongoni mwa vijana ambapo pia ililihusisha shindano la vazi la kitenge na kujitolea (KAV), tukio hilo ni kuhamasisha ili watu watambue kwamba suala la kujitolea ni sawa na jambo la kila siku kama kuvaa vazi la kitenge.
Mmoja wa wafanyakazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kujitolea (UNV), (kulia) akitoa maelekezo kwa mmoja wa vijana aliyohudhuria katika warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV) iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kazi ya kujitolea miongoni kwa vijana.

Mtendaji Mkuu wa Chama cha Vijana wa Shirika la Umoja wa Mataifa (YUNA), Arafat Bakar akitoa maelezo kuhusu YUNA inavyofanya kazi kwa jamii ya Tanzania na hususani vijana katika warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV).
Mkurugenzi Mtendaji wa Young Tanzanian for Community Prosperty, Alfred Magehema akitoa maelezo kuhusu taasisi yake na jinsi taasisi yake inavyofanya kazi katika kuisaidia jamii.
Mmoja wa Maafisa wa Raleigh Tanzania, Rose Mmbaga akitoa ufafanuzi kuhusu taasisi yao jinsi ilivyoanza, wanavyofanya kazi na mafanikio waliyoyapata mpaka sasa.
Meneja wa Taasisi ya AIESEC Tanzania, Onome Ahorituwere akitoa ufafanuzi kuhusu kazi zinazofanywa na taasisi hiyo katika warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV).
Pichani juu na chini baadhi ya vijana walioshiriki katika warsha ya Kitenge Africa Volunteerism (KAV) iliyokuwa na lengo la kuhamasisha kazi za kujitolea miongoni mwa vijana hao.
Washiriki wa warsha ya Kitenge X Africa X Volunteerism (KAV), wakiwa katika picha ya pamoja.
chanzo;michuzi blog

Mbunge wa Chalinze akabidhi vitabu 3438 vya shule za msingi 105 na sekondari 17

Mbunge wa Jimbo la Chalinze,Mh. Ridhiwani Kikwete, leo amekabidhi vitabu 3438 vya shule za Msingi 105 na Sekondari 17 vyenye thamani ya Shilingi Milioni 68,760,000, kwa Afisa Elimu wa Halmashauri ya Wilaya ya Chalinze, Mkoani Pwani. 

Makabidhiani hayo yamefanyika mapema leo asubuhi kwenye Shule ya Sekondari ya Mdaula.

Saturday 6 February 2016

Marafiki wa shirika la kiraia la TACOMO wawaona wagonjwa Hospitali teule Mbeya Vijijini

Baadhi ya marafiki wa Shirika la kiraia la Tanzania Community Media Organization (TACOMO), wkiwa na baadhi ya viongozi wa shirika hilo katika Hospitali ya Ifisi Mbalizi Mbeya Vijijini, wakiingia kuwaona wagonjwa.

Mchango wa kuwaona wagonjwa ulitoka mifukoni mwa marafiki wa shirka hilo baada ya kuhamasishwa na shrika umuhimu wa kuwaona wenye mahitaji.

TACOMO inashiriki katika masuala ya usafi wa miji Tanzania Bara

Kuli ni Mkurugenzi mtendaji wa Maendeleo ya wilaya ya Mbeya, Upendo Sanga, akijumuika na wananchi wa mji mdogo wa Mbalizi kufanya usafi. Aliyeshika simu ni Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Community Media Organization (TACOMO), ndugu Gordon Kalulunga.

Wape nafasi wanawake watoe sauti zao


TACOMO; Waliojifungua watoto wenye vichwa vikubwa njooni

SHIRIKA lisilo la kiserikali la Tanzania Community Media Organization (TACOMO), limewataka wazazi wote wenye watoto waliozaliwa wakiwa na vichwa vikubwa wasiozidi miaka miwili Tanzania bara, wajitokeze na watagharamiwa gharama za matibabu.

Shirika hilo ambalo lina makao makuu mkoani Mbeya na linafanya kazi Tanzania bara, limesema kuwa kansa ya watoto inatibika hivyo wazazi wasiwafiche watoto wao na kwamba shirika hilo kwa sasa linaendesha mradi wa kuwasaidia watoto wenye matatizo hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Mbeya leo, Mkurugenzi wa shirika hilo ndugu Gordon Kalulunga, amesema shirika lao kwa kila mzazi atakayejitokeza atagharamiwa nauli ya kutoka popote Tanzania Bara na kuelekea katika Hospitali ya Taifa Muhimbili au Bugando Jijini Mwanza, ambapo akifika huko ataunganishwa moja kwa moja na marafiki wa shirika hilo ambao watampokea na mtoto kufanyiwa vipimo vya awali kisha upasuaji.

"Tafadhali, naomba vyombo vya habari tusambazieni taarifa hizi kwa watanzania wote. Kwanza kabisa tunaomba kila mwananchi atambue kuwa kuna shida duniani na tunapaswa kujaliana hivyo tunaomba michango ya hali na mali ya kuwawezesha watoto wenye matatizo ya vichwa vikubwa na kuwasafirisha pia maana matibabu yanatolewa bure katika hospitali ya Bugando Mwanza na Muhimbili Jijini Dar e Salaam" alisema Kalulunga.

Alisema mwenye taarifa ya mtoto aliyezaliwa akiwa na kichwa kikubwa anaweza kuwasiliana moja kwa moja na uongozi wa shirika hilo kwa namba 0765 615858 na kwa marafiki ambao wanaguswa na suala hili la kusaidia wahitaji wanaweza kuchangia michango yao kwa namba 0754 440 749/0655 440 749 au 0765 615858 na kwa Akaunti benki ya NMB 

JINA LA AKAUNTI:  TANZANIA COMMUNITY MEDIA ORG
NAMBARI YA AKAUNTI: 62510007257
JINA LA BENKI: MICROFINANCE BANK (NMB)
JINA LA TAWI: USONGWE BRANCH